siku
moja baada ya kushiba sima yangu baraabara,nilikaa
chini ya kivuli na kushkuru ile neema ya shibe aliyo nipa
mwenyezi mungu.
Baadae nilikaa
nikatafakari na kujiuliza je haya maisha ni nini
hasa? nikushiba sima na kuteuka tu au kuna la ziada?
Lakini na
kumbuka wakati mmoja nilikuwa nasoma kitabu kilichoitwa
visa vya manabii,basi nilisoma kisa cha nabii mmoja aitwae IBRAHIM
(A.S) nabii huyu wakati wa ubarubaru wake,siku moja alikaa akajiuliza
mimi mungu wangu ni nani?wakati akijiuliza maswala haya ilikuwa ni
wakati wa usiku mwezi ulikuwa iki'ara sana,basi yeye akasema mungu
wake ni ule mwezi.
Asubuhi kulipo
pampazuka jua lilichomoza na mwezi ukapotea,basi akasema
mungu wangu ni hili jua ulipo fika wakati wa usiku lile jua nalo likapotea
tena,kufikia hapo akasema mimi sipendi mungu wa kuja na kupotea,kwa hivyo
yeye akaamua ya kwamba mungu wake ni yule alieumba hivyo vitu vyote.
kutokana na
kisa hichi kifupi na mimi niliwahi kujiuliza na bado naendelea
kujiuliza haya maisha hasa ni nini? na kukamilika kimaisha ni nini?
kulingana na uchache wa ilmu yangu nimepata kujua vitu kadha wa kadha
kuhusu maisha.
Na maswala
haya nadhani siko peke yangu kwani nimepata kujua ya kwamba
wako watu wengi ambao nao pia wafanya utafiti wao ili kuweza kujaribu
kutatua kitendawili hichi cha maisha kwa kuimba nyimbo za maisha na
mengi mengineo.
Tukianza na
muumba wetu S.W.T amesema haya maisha ya dunia nistarehe chache
inayo tuhadaa sisi waja wake na ambayo twaipenda sana.
Twayapenda
vipi?kila binadamu anapenda awe na nyumba ya kifahari,gari kubwa,
pesa nyingi na uwezo mkubwa maishani uwezo wa kuweza kufanya yale anayo
taka kufanya.
Ingawa kwenye
maandiko mwenyezi mungu ametuahidi pepo na mengi mazuri lakini
ni wachache wetu ambao wana aari ya kutaka hiyo pepo sababu kila unae
muuliza
yeye ataka pesa,nyumba kubwa na kadhalika.
Wakati mwengine
nilikuwa nafuga kuku ifikapo asubuhi wale kuku huwa wnaleta
vurugu mpaka wafunguliwe ili watoke nje wakaendelee na shughuli zao za
kutafuta
riziki .
Kwa mfano
huu wa hawa kuku pia ikawa kama somo kwangu,najiuliza je,ina maana
maisha ni lazima kila kiumbe kutoka kikatafute?ndio maana watu kila asubuhi
lazima
watoke nje wakatafute na warudi jioni waje wapumzike baada ya siku nzima
ya maangaiko
katika nafsi yangu nikasema yaonekana ni hivyo.
wakati mwengine
nilipokuwa nasoma Quran nilipitia aya inayosema mwanadamu ni bora
kuliko wale viumbe wengine lakini asipotumia ile akili yake aliyopewa
na S.W.T basi yeye
huwa chini kuliko wale walio chini,kwa aya hiinikatafakari kwa kina nikasema
haya maneno
ni kweli.Sababu kulingana na maono yangu niki chukua mfano wa hawa viumbe
wengi kama
kuku huwa asubuhi wanatoka kwenda kutafuta riziki yao bila kubugudhu kiumbe
mwengine
Lakini sisi
binaadamu kuna wengi wetu hawataki kutoa jasho lao wao hutaka amshikie
mwanadamu mwenziwe ma panga ampige na amnyang'anye kila kilo chake,ambapo
mimi hata
siku moja katika maisha yangu sijaona hayo kama kuku kumshikia mwenzie
panga amnyang'anye
Je tukitafakari
wanadamu maisha ni nini?ni kupigana mapanga au ni nini?
|